Staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amefunguka kuwa kwa sasa
hatakubali tena kusumbuliwa na wanaohoji juu ya maisha yake mapya ya
wokovu.
Staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’.
Akizungumza na paparazi wetu, Mainda alisema mwanzoni alikuwa anapata
shida sana kuishi na watu kwani yeye kama msanii kila anachofanya watu
wanachukulia ndivyo sivyo na hata katika wokovu pia wanahoji kama
atauweza kitu ambacho anaamini hatotetereka.
“Nimejifunza vitu vingi sana kutokana na ustaa wangu, watu wengi
wananiangalia kwa jicho lingine wanataka kuona je Mainda ana mabadiliko
gani baada ya kuokoka? Ninapoteleza kama mwanadamu utasikia watu
wanasema mimi si mlokole, siwajali kwa sasa,’’ alisema Mainda.
No comments:
Post a Comment