Amina Ibrahim (27), mkazi wa Kimara jijini Dar anayeshikiliwa kwa kesi ya kumuua 'mwanaye'.
MKAZI wa Kimara Amina Ibrahim (27), amepandishwa Kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Jijini Dar es Salaam akikabiliwa na
shitaka la kumuua mtoto wa kambo.
Akisomewa kosa hilo leo mbele ya Hakimu Amalia Mushi, Wakili wa
Serikali Faustine Sylivester, alidai kuwa tukio hilo lilitokea Juni 18
mwaka huu huko Kimara, Wilayani hapo.
Sylivester alidai kuwa mshitakiwa alikuwa akiishi naye na ndipo
alipoamua kumuua mtoto huyo ajulikanaye kwa jina la Munir Dodi (6),
wakati akifahamu kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai kufanya hivyo kwa
mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mshtakiwa hakutakiwa kujibu kitu chochote kutokana na kosa lake kwani
Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo, hivyo kesi
imeahirishwa hadi Agosti 15 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
No comments:
Post a Comment