STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond'
amezidi kupasua anga la kimataifa kwa kuhudhuria Tuzo za BET 2014, Los
Angeles, Califonia nchini Marekani usiku wa kuamkia leo na kuwa gumzo
nchini humo.
Kwenye tuzo hizo, Diamond alikuwa akiwania Tuzo ya Msanii Bora wa
Kimataifa kutoka Afrika 'Best International Act: Africa' ambayo
ilichukuliwa na msanii Davido kutoka nchini Nigeria.Licha ya kukosa tuzo hiyo, Diamond alikuwa gumzo kwa wasanii wengi nchini humo kwa kuonekana kumkubali na kuonesha dalili njema za kuweza kufanya naye kazi kwani alipata bahati ya kubadilishana namba na baadhi ya wasanii wenye majina makubwa.
Miongoni mwa fursa alizozipata Diamond katika tuzo hizo ni pamoja na kupiga stori na rapper mahiri wa Marekani, Cornell Iral Haynes 'Nelly', kufanya mahojiano na host aliyekuwa akiongoza mahojiano na mastaa katika Red Carpet ya tuzo hizo, Karrueche Tran ambaye ni mpenzi wa staa wa muziki Chris Brown na kukaa kwa ukaribu na mastaa wa dunia waliopokea tuzo usiku wa kuamkia leo.
Kuonyesha kuwa staa huyo kapiga hatua kubwa, aliandika kupitia ukurasa wake wa Instagram hivi:
Na baada ya kukutana na kupiga stori na Nelly alitupia hivi kupitia akaunti yake ya Instagram:
No comments:
Post a Comment