Mheshimiwa Shukuru Kawambwa
Baada ya
Waziri wa Elimu na Mafunzo, Dr Shukuru Kawambwa, kuzushiwa kifo
imeelezwa na ndugu zake kuwa ni mzima wa afya na anatumikia taifa.
Mapema
Jumanne uliibuka uvumi kupitia baadhi ya mitandao kwamba Waziri huyo
ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Bagamoyo(CCM) alikuwa ameaga dunia.
Lakini mbunge wa Chalinze, Ridhwan Kikwete akajitokeza kukanusha habari hizo kupitia ujumbe mfupi.
Ridhwan alisema: “Ndg
Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba ya CCM-Bagamoyo
na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta kwenu masikitiko
yetu kwa niaba ya Chama na familia ya mheshimiwa mbunge Shukuru Jumanne
Kawambwa kutokana na usumbufu ambao umesababishwa na habari zinazoenezwa
mitandaoni kwamba mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na umauti akiwa njiani
anaelekea Mwanza,” alibainisha Kikwete.
“Mheshimiwa
Shukuru Jumanne Kawambwa yupo nchini Canada akitimiza majukumu yake.
Hivyo watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa usumbufu uliotokea
na kwamba mheshimiwa mbunge yuko na afya njema na utekelezaji wa
majukumu unaendelea kama kawaida”, alikamilisha Ridhiwani Kikwete ambaye ni mbunge wa Chalinze (CCM).
No comments:
Post a Comment