Thursday, June 26, 2014

MAJONZI: MWILI WA SISTA ALIYEPIGWA RISASI WAAGWA JIJINI DAR LEO

Masista wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Sista Cresensia Kapuli aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi Juni 23, 2014.

 Sista Brigitte Mbaga aliyekuwa na marehemu Cresensia Kapuli eneo la tukio siku alipopigwa risasi akiwa na simanzi.

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond H. Mushi aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick.

 Mwakilishi wa mama watawa wakuu wa shirika la malkia kutoka Mbeya akilia kwa uchungu.

 Jeneza likiwekwa ndani ya gari tayari kwa safari ya Mbeya kwa maziko.

SISTA Cresensia Kapuli aliyepigwa risasi Jumatatu Juni 23, 2014 maeneo ya Ubungo, River Side na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi hatimaye ameagwa katika Parokia ya Makoka, Kibangu jijini Dar.
Mwili wa marehemu umeagwa na umati wa watu wa rika zote wakiwemo viongozi wa dini na serikali. Baada ya kuagwa, mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda jijini Mbeya kwa ajili ya maziko yatakayofanyika Juni 28, 2014.
Bwana ametoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!

No comments:

Post a Comment