Askari wa jeshi la serikali la Sudan Kusini wakiwa doria.
Umoja wa Mataifa umeomba mchango wa dola bilioni moja kuwasaidia watu walioathirika na vita Sudan Kusini.
Baada ya miezi sita ya mapigano mkuu wa misaada
wa Umoja wa Mataifa, Toby Lanzer, amesema watu milioni 7 wako katika
hatari ya njaa na magonjwa.
Alieleza kuwa wengi waliokimbia makwao wanaishi
kwenye matope kwa sababu msimu wa mvua umeshaanza; malaria imezagaa na
kipindupindu kimezuka.
Awali juma hili serikali ya Sudan Kusini na
wapiganaji walikubaliana kusitisha vita, lakini siku za nyuma
makubaliano kama hayo yalikiukwa haraka.
Hivi ndivyo maisha yalivyo kwa silimia kubwa ya raia wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment