Friday, June 13, 2014

NAY WA MITEGO AWEKA HESHIMA MJINI.... AHAMIA KWENYE MJENGO WAKE WA KIFAHARI, HABARI NA MAPICHA SOMA HAPA

Alipoanza kwa kutoa ngoma yake iliyomtambulisha kwenye gemu ya Nasema Nao, hakuna aliyetegemea kwamba Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ aliye chini ya Brand ya Mkong’oto Jazz Band anaweza kufika mbali na kupata mafanikio makubwa kama aliyonayo leo.

 Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa pembeni ya ndinga yake mpya aina ya Nissan Murano yenye thamani ya milioni 35.

Wengi walimuona kama amevamia gemu bila kujipanga huku akielekeza nguvu kubwa kuandika mashairi ya kuwaponda wasanii wenzake, wanasiasa na watu maarufu huku akitangaza bifu na wasanii kibao.
Kumbe mchizi huyo anayependa pia kuitwa True Boy, alikuwa ameona mbali na kuamua kutoka kwa staili ya kivyakevyake, akazidi kukomaa kwenye gemu na kuzidi kujizolea mashabiki kibao waliokuwa wakiizimia kinoma staili yake ya kuimba kibabe.

 Huu ni mjengo wa Nay wa Mitego uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 120.


Ngoma ya Muziki Gani aliyofanya na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ikaleta mapinduzi makubwa katika muziki wake, akaanza kupendwa hata na wale ambao awali hawakuwa wakimkubali.
Muvi likaendelea huku umaarufu wake ukizidi kupaa, akafunga kazi kwa kuachia ngoma ambayo bado inaendelea ‘kubang’ mpaka sasa, Nakula Ujana. Akapata shoo zisizo na hesabu na kubwa zaidi, akalamba mkataba wa pesa ndefu kwenye kampuni moja ya simu za mkononi, na sasa anakula ujana kinomanoma.

 Nay wa Mitego kama kawaida yake akila ujana katika pozi kali .

 MJENGO WA MAANA
Ndani ya kipindi kifupi tu ambacho True Boy amepanda kwenye chati, tayari anamiliki mjengo wa maana uliopo Kimara Baruti jijini Dar ambao kwa mujibu wake, umegharimu zaidi ya shilingi milioni 120 (tazama picha), ukiwa na vitu kibao vya kisasa ikiwemo fensi ya umeme, CCTV Camera na fenicha za hatari.
“Mjini hakuna baba mwenye gari bali kuna baba mwenye nyumba, heshima inaanzia kwenye nyumba, nilipopata mkwanja, jambo la kwanza lilikuwa ni kwenye mjengo. Hii nyumba niliinunua kwa mtu ikiwa ya kawaida kabisa, ikabidi niifumue na kuanza upya kujenga ili kupata kitu nilichokuwa nakitaka.

 Nay wa Mitego akiwa na mkali mwingine wa Bongo Fleva, Abdul Nassib Diamond.

 “Najivunia sana kuwa na nyumba ya maana, hata kesho nikifa najua nitazikwa kwangu. Ninazo nyumba nyingine kadhaa, Mungu akitujaalia mwezi Oktoba nitaitambulisha nyumba yangu nyingine ambayo itakuwa imekamilika,” alisema Nay wa Mitego.
MKOKO WA NGUVU, BAJAJ 2
 Ukiachilia mbali mjengo huo ambao kwa mara ya kwanza Nay ameutambulisha kupitia Gazeti la Ijumaa, pia mchizi amevuta ndinga mpya, Nissan Murano ambayo thamani yake ni shilingi milioni 35.
“Nimenunua Nissan Murano mpya kutoka Showroom, nafikiri bei yake inafahamika, milioni 35 cash.
Pia nimenunua Bajaj mbili mpya kwa ajili ya wadogo zangu ziwe zinawasaidia mambo madogomadogo. Kila moja nimenunua shilingi milioni 6. Sitaki wadogo zangu wapate shida kabisa, nataka wajishughulishe.
“Namshukuru sana Mungu kwani sasa nayaona matunda ya jasho langu, nawashukuru mashabiki na wadau wanaonipa shoo, najisikia furaha sana, ukiwa na nyumbani kwako raha sana, namshukuru mama kwa kunifundisha maisha na namshukuru pia demu wangu, Siwema,” alisema Nay.
Kufuatia mafanikio hayo makubwa aliyoyapata ndani ya kipindi kifupi, Nay wa Mitego anaingia katika orodha ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya wenye mafanikio makubwa. Big up True Boy!



No comments:

Post a Comment