SIKU chache baada ya tuhuma za ubakaji na mzozo wa familia ya mwimba
Injili mahiri nchini, Flora Mbasha na mumewe, Emanuel Mbasha, mambo
mengine yameibuka.
Mwimba Injili mahiri nchini, Flora Mbasha
Yaliyoibuka safari hii ni taarifa kwamba, juzikati, Flora alivamiwa
na watu wasiojulikana nyumbani kwake, Tabata Kimanga jijiini Dar dakika
chache baada ya yeye kuingia na gari akitokea mafichoni anakoishi kwa
sasa.
Kwa mujibu wa chanzo, siku ya tukio
ilikuwa saa 9.15 alasiri ambapo Flora aliingia nyumbani kwake na
kufunguliwa geti kubwa kisha kuingiza gari ndani na geti kufungwa tena.
“Flora aliingia na gari akitokea hotelini anakoishi kwa sasa. Alikuwa
ameshaingia na geti likafungwa. Ghafla, watu wakafika na kugonga geti
hilo kwa nguvu huku wakisema watalibomoa geti kama wenyeji hao
hawatafungua,” kilisema chanzo.
Mwimba Injili mahiri nchini, Flora Mbasha akiwa na mumewe, Emanuel Mbasha,
Chanzo kikazidi kudai kwamba, ilibidi Flora apige simu polisi ili wafike kumuokoa yeye na familia yake.
“Polisi wawili walifika haraka sana wakiwa na bunduki na kukuta wale
watu wamekimbia maana walimsikia Flora akiongea na polisi kuomba msaada.
“Lakini polisi wenyewe ilibidi watumie nguvu kubwa kugonga geti na
kujitambulisha ndipo akatokea Flora na kuchungulia nje kupitia dirisha
dogo. Alipowaona polisi akafungua mlango,” kilisema chanzo hicho.
Akihojiwa na polisi hao, Flora alisema watu hao walikimbia na hakuwajua kwa sura wala hawakujitambulisha ni akina nani.
Alizungumza na gazeti hili baada ya tukio, Flora alisema: “Unajua kwa
sasa nina hofu sana na nilihisi wale watu walikuwa wakinifuatilia kwa
karibu kila sehemu, sasa naogopa kuendelea kuishi hapa, wanaweza kurudi
na sijui lengo lao.”
Hata hivyo, baada ya askari hao kuondoka katika eneo hilo, Flora naye
aliingia kwenye gari lake akiwa na mdogo wake na kuondoka.
Mume wa
Flora, Mbasha naye yupo mafichoni baada ya kudaiwa kumbaka binti wa
miaka 17 ndani ya nyumba yao huku utata ukitawala kuhusu ukweli wa tukio
hilo ambalo limeigawa jamii.
GPL
No comments:
Post a Comment