Maafisa wakuu katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo
wanasema kuwa makabiliano makali yalizuka mapema leo kati ya wanajeshi
wa DRC na wanajeshi wa Rwanda.
Waziri wa mawasiliano, Lambert Mende, anasema
kuwa makabiliano hayo yaliendelea kwa muda na kuendelea kwa saa kadhaa
katika eneo la mpakani kati ya nchi hizo mbili.Hadi sasa hapajakuwa na tamko lolote kutoka kwa upande wa Rwanda.
Serikali ya Rwanda imetuhumiwa na Umoja wa Mataifa kwa kuhusika na mzozo unaotokota katika mashariki ya Jamhuri ya Congo.
Rwanda imekanusha madai hayo.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment