Watu watatu wamekufa na wengine kumi wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noha kupasuka tairi ya nyuma na kubingirita mara tatu katika kijiji cha Januka manispaa ya Singida.
Akithibitisha kitokea kwa vifoo hivyo mganga
mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida daktari Deogratias Banuba
amesema wamepokea maiti mbili wakiwa wamesha fariki eneo la tukio
akiwemo dereva wa Noha bwana Enock Mbaga, binti Ajira Juma na maiti
nyingine ya Bi Tatu Bunku ambaye alikuwa herd mistres Ngimu sekondari
amefia katika hospitali ya mkoa wa Singida .
Daktari Banubasi amesema majeruhi kumi wamepatiwa
huduma ya kushonwa sehemu mbalimbali za miili yao na wanaendelea na
matibabu ,pia hakuna majeruhi ambaye atapatiwa rufaa .
Mmoja wa majeruhi akiongea kwa shida huku akiwa
amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida bwana Ramadhani Mlenga
amesema gari halikuwa katika mwendo wa kasi na gafla likaacha njia na
kupinduka mara tatu.ITV
No comments:
Post a Comment