Leo mwanadada Blandina Chagula maarufu kama Johari anasherehekea
siku yake ya kuzaliwa. Tuliweza kupata nafasi ya kufanya interview na
mlimbende huyu katika siku yake hii kubwa ya leo ambapo pamoja na mambo
mengi alitoa ujumbe huu kwa watu wote ma mashabiki wake wote.
“Napenda kuwaambia wapenzi wa filamu nchini kuwa kwanza kabisa
nashukuru kwa support yenu kwa kununua kazi za nyumbani, kwani bila
ninyi Johari asingekuwa Johari anayeonekana sasa. Napenda kuwashukuru
wazazi wangu walionizaa kwani bila wao nisingefika hapa nilipo leo na
pia mashabiki wangu wasipate wasiwasi kwani kila siku tunzaidi kupata
mawazo mapya ya kuboresha filamu zetu hivyo wakae tayari kupata burudani
zaidi na zaidi toka kwetu. Asanteni Sana”
Hongera sana dada Johari kufikia siku ya leo. Mungu akupe miaka mingi hapa Duniani.
No comments:
Post a Comment