Sunday, June 15, 2014

KIONGOZI WA UPINZANI SUDAN SADIQ AL MAHDI AACHIWA HURU

Sadiq Al- Mahdi

Wakuu wa Sudan wamemuachilia huru kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Sadiq al-Mahdi, ambaye alikamatwa mwezi May kwa mashtaka ya kuchochea chuki dhidi ya taifa.
Adhabu ya mashtaka hayo yanaweza kuwa kifo.
Bwana al Mahdi, ambaye anaongoza chama cha Umma, alilalamika juu ya sera za serikali kuhusu Darfur na alishutumu wanajeshi wa serikali kuwa wanakiuka haki za kibinaadamu, pamoja na ubakaji.
Waziri wa Habari wa Sudan, Yasser Youssef, alisema Sadiq al-Mahdi aliachiliwa huru kufuatana na sheria za nchi, lakini hakueleza zaid

BBC

No comments:

Post a Comment