IMEBAINIKA kuwa miongoni mwa wale wanawake 20 waliodai
kufanyishwa ngono na waganga wa kienyeji ‘sangoma’ ili kupata ujauzito
baada ya kukaa muda mrefu bila watoto, wamo wake wa vigogo Bongo, imebumbuluka.
Kamanda Kiondo akielezea kuhusu uhalifu wa Sangoma walionaswa kwa kufanya ngono na wake wa vigogo.
Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu kwa baadhi ya wanawake hao
umebaini kuwa, waume wao wanafanya kazi katika nyadhifa za juu
serikalini, wengine ni wastaafu na kwamba waume hao hawajui
kinachoendelea.
Kwa mujibu wa mwanamke mmoja (jina lipo), katika sakata hilo kuna
wake wa maprofesa, kanali mstaafu wa JWTZ na mmoja ambaye mume wake
aliwahi kuwa kamanda wa polisi wa mkoa (RPC) ambaye kwa sasa naye ni
mstaafu.
...Kamanda Kiondo akizidi kuonyesha vifaa vilivyokuwa vikitumiwa na waganga hao wa kienyeji.
Mwanamke huyo alizidi kudai kuwa, ndoa moja katika hizo ilivunjika
baada ya mume kubaini kuwa, mkewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na
mmoja wa sangoma hao.
‘KUFULI’ ZILISHATUMIKA
Uchuguzi zaidi ulibaini kuwa zaidi ya nguo
za ndani ‘kufuli’ za wanawake zaidi ya 20 zilizokutwa na polisi kwa
sangoma hao maeneo ya Tandika jijini Dar es Salaam zilikuwa
zimeshavaliwa hivyo hakukuwa na mpya jambo lilionesha kuwa, zilivuliwa
wakati wa tukio linalodaiwa lilikuwa na kutengezea dawa.
Baadhi ya watuhumiwa wa sakata hilo.
KWA NINI WALITOA TAARIFA POLISI?
“Sisi tuliamua kutoa taarifa
polisi kwa sababu tumekuwa tukifanya ngono na wale waganga kwa muda
mrefu bila kupata ujauzito na mbaya zaidi tulishatumia mamilioni ya
pesa baada ya kuuza mali zetu, zikiwemo nyumba,” alisema mwanamke huyo
nje ya kituo cha polisi.
Wanawake hao ambao hawakupenda majina yao yatajwe kwa kuhofia waume
zao kujua, walisema ni kweli baadhi yao wamekaa katika ndoa kati ya
miaka nane hadi 10 bila kupata watoto wala mimba zilizoharibika.
Kamanda Kiondo akionesha
baadhi ya nguo za ndani, 'kufuli' zilizokutwa kama ushahidi kwa baadhi
ya wanawake waliofanyishwa ngono na sangoma hao.
Hata hivyo, baadhi yao walirudishiwa fedha zao baada ya Kamanda Kiondo kuwabana waganga hao.
KAULI YA RPC
Wiki iliyopita Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke chini
ya Kamanda, SACP Englibert Kiondo liliwatia nguvuni sangoma wawili
wakiwa na matunguli na zana nyingine za kuagulia binadamu.
Kamanda Kiondo akikusanya tunguli zilizotumiwa na waganga hao wahalifu tayari kwa kuzichoma moto mbele ya wahandishi wa habari.
Vitu hivyo viliteketezwa moto kwenye Kituo cha Polisi Temeke mbele ya waandishi wa habari.
“Ninaamini kuwa kwa vitendo hivyo vya kujamiiana ni hatari na huu ni
ubakaji, kwani kuna uwezekano wa kuambukizana maradhi mbalimbali
ikiwemo Ukimwi, kwa hiyo hizi zana nazichoma moto,” alisema Kamanda
Kiondo.
...Tunguli zikiteketezwa kwa moto.
Waliokamatwa katika zoezi hilo ni Juma Mohamed (32) na Abdallah Musa (25) ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo.
GPL
No comments:
Post a Comment