Mwandishi mkuu wa Mbeya Yetu Blog, Joseph Mwaisango.
TONE MULTIMEDIA GROUP ambao ni wamiliki wa Mtandao wa Mbeya yetu Blog , Tunapenda Kuungana na wadau wetu wote Kumpongeza Bwana Joseph Mwaisango
ambaye ndiye Mwandishi Mkuu wa Blog hii ya Mbeya yetu na Mmoja wa
wakurugenzi wa Tone Multimedia Company Limited (TMCL) ambao pia ni
wamiliki wa Blogs za Mikoa Tanzania, Tone Radio-Tz , This Day Magazine, Stay In Tanzania(Tanzania Tours) , Tone Tube Tz , Matukio na Wanavyuo na Watanzania waishio nje ya Nchi kwa kutimiza miaka yake kadhaa siku ya Leo.
Tunapenda kumpa Hongera sana kwa kazi
nzito ambazo anazifanya ili kuwaletea wadau habari zilizo sahihi na za
uhakika zaidi kutoka pande zote za Mkoa wa Mbeya, Pia tunamuombea kwa
Mungu ampe siku nyingi zaidi , Afya Njema na aendelee kuchapa kazi zaidi
na zaidi bila kusahau kuongeza Ubunifu zaidi.
Pia katika Hili tunapenda kuwashukuru
wadau Mbali mbali wa Habari wakiwemo Bloggers wote wa Tanzania,
Magazeti, Radio na TV kwa kuendelea kuonesha ushirikiano mkubwa ili kazi
ziendelee kwa ufanisi mkubwa
Mwisho tunapenda kumshukuru kila mmoja
wetu ambaye ni mdau mkubwa wa Blog ya Mbeya yetu, wote tupo pamoja
katika kusherekea siku hii ya leo.
No comments:
Post a Comment