Saturday, May 10, 2014

SOMA HAPA JINSI MC ALIVYOZUA BALAA KWENYE MSIBA WA KADA WA CHADEMA IRINGA MJINI.

Marehemu Gervas Kalolo enzi za uhai wake, hapa akiwa na Mbunge wa Iringa mjini kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010

MAZISHI ya kada maarufu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Gervas Kalolo yatikisa mji wa Iringa baada baada ya magari zaidi ya 100 na boda boda na bajaji zaidi ya 200 kupamba msafara wa mazishi hayo jana

Mazishi hayo ambayo yaliongozwa na mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa yalionyesha kuvunja rekodi ya mazishi yaliyopata kufanyika katika mji wa Iringa .

Awali utaratibu wa mazishi hayo ulitaka kuvurugika kutokana na vijana wa Chadema kuanza kuzomea makaburini wakati Mc wa mazishi hayo wakati akitambulisha taratibu za watoa salam mbali mbali na kumtaka mwakilishi wa chama cha mapinduzi (CCM) huku akishindwa kumtaja mwakilishi wa Chadema na kuishia kusema kutakuwa na mwakilishi wa chama bila kutaja jina la chama husika .

Hata hivyo baada ya MC huyo kufuatwa na diwani wa Chadema kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi na kumlazimisha kutaja jina la Chadema badala ya kuishia kutaja chama bila jina lake ,ndipo alipolazimika kuepusha vurugu kwa kutaja jina la chama cha Chadema na kupelekea kuibuka kwa shangwe katika msiba huo.

Mbali ya kuibua shangwe kwa kuimba wimbo wa Chadema Chadema alisimama mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Msigwa ambae pia alishangiliwa kwa nyimbo hizo za Chadema .

Akizungumza katika mazishi hayo mbunge Msigwa mbali ya kumshukuru mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi na viongozi wa CCM kwa kushirikiana na chama katika mazishi hayo bado alisema kuwa kimsingi siasa katika msiba huwekwa kando.

Mbunge Msigwa alisema kuwa kiongozi yeyote na mtu yeyote mchango wake hupimwa kwa matendo yake na kuwa umati wa wananchi waliojitokeza katika mazishi hayo ni wazi kuwa Kalolo alikuwa ni kiongozi wa mfano katika jamii na kuwa Chadema itamuenzi kwa kusimamia msimamo wake wa kupinga ufisadi .

Kwa upande wake mwakilishi wa CCM katika mazishi hayo Shadrack Mkusa alisema kuwa Kalolo ambae alipata kuwa diwani wa kata ya Miyombini Kitanzini kabla ya kushindwa katika kura za maoni na kujiunga na Chadema.

Alisema kuwa Kalolo anakumbukwa kwa mengi ambao amepata kuyafanya likiwemo la kusimamia hoja zake katika vikao vya madiwani pamoja na kujitolea kusaidia watoto yatima katika kata yake.
 
 Msafara wa Magari, bajaji na bodaboda ukielekea kwenye mazishi ya Gervas Kalolo.

Jeneza lenye mwili wa Gervas Kalolo likipelekwa makaburini.

 Mbunge wa Iringa Mch. Peter Msigwa mjini akiweka shada la maua kwenye kaburi la Gervas Kalolo.

Hapa ndipo ilipoishia safari ya maisha ya duniani ya Gervas Kalolo. Apumzike kwa amani.

No comments:

Post a Comment