Friday, May 9, 2014

SOMA HAPA JINSI DC. MRISHO GAMBO ALIVYOMLIPUA MWENYEKITI WA CCM TANGA

WAKATI PIRIKA ZA KUJIPANGA KUWANIA URAIS NDANI YA CCM ZIKIZIDI KUPAMBA MOTO, SOMA HAPA JINSI MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO ALIVYOMLIPUA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA TANGA MH. HENRY SHEKIFU.

Labda leo niseme japo haikuwa nia yangu kusema. Bw. Henri Daffa Shekifu ( chair CCM Tanga) aliniomba nimuunge mkono Mhe. Lowasa kwenye kugombea Urais 2015. Nikamjibu kuwa hiyo siyo kazi niliyopewa Korogwe.

Toka siku hiyo visa vikaanza! Diwani anaemsema kesi yake iko mahakamani kwa kuchochea watu wakachome maboma na mazizi ya wafugaji!

Yeye jana kasema Bungeni, mimi si mbunge, natumia forum hii!


DC. Mrisho Gambo akiwa na Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta
Mrisho Gambo akisalimiana na rais Jakaya Kikwete.

Mrisho Gambo anaonekana kuwa mmoja kati ya wakuu wa wilaya vijana wenye uwezo mkubwa sana wa kiutendaji na kusimamia shughuli za serikali kuliko ilivyo kwa wakuu wa wilaya na mikoa wengi ambao huishia kupiga siasa katika nafasi wanazopangiwa kufanya kazi. Blogu hii inamuunga mkono DC. Mrisho Gambo katika juhudi zake za kusimamia kile kilichompeleka Korogwe na kumtaka aendelee na msimamo huo huo kwa manufaa ya watu wa Korogwe na taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment