ZILIPENDWA wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’,
Penniel Mungilwa ‘Penny’, amefunguka kuwa hataki kumsikia mpenzi wake
huyo wa zamani kwa madai kuwa amefungua ukurasa mpya wa uhusiano na mtu
ambaye hata hivyo hakuwa tayari kumweka wazi.
Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’.
Penny alisema hayo hivi karibuni jijini Dar wakati akizungumza na gazeti
hili lililotaka kujua anazungumziaje tuzo saba za Kilimanjaro
alizojizolea Diamond ambapo majibu yaliyopatikana yalikuwa:
“Wanaotakiwa kuzungumzia hili ni mkewe na ndugu zake, mimi sitaki.”
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Alipoulizwa mke wa Diamond ni nani alisema: “Mnamjua” na kuicha historia
ikibaki kuwa Penny na msanii huyo waliwahi kuwa katika mapenzi mazito
ya njiwa kabla ya kumwagana na mwanamuziki huyo kumrudia mpenzi wake wa
zamani, Wema Sepetu, ambaye mwenyewe anapenda aitwe mke mtarajiwa.
Hahahaha!
No comments:
Post a Comment