MSHTUKO! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Jeshi la
Polisi mkoani hapa, limelazimika kuwaita wafanyakazi wa chumba cha
kuhifadhia maiti (mochwari) wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kushuhudia
mwili wa mtu aliyekutwa amekufa kwenye kichaka jirani na ofisi za makao
makuu ya jeshi hilo.
Wananchi wakiushuhudia mwili wa Juma Mbega ukiwa kwenye maji.
Kwa mujibu wa polisi, mwili wa mtu huyo aliyefahamika kwa jina la
Juma Mbega (46) ulikutwa kwenye kichaka ukiwa umeharibika vibaya na
kutoa harufu kali huku ukizungukwa na wadudu, nusura polisi wenyewe
watoke nduki.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Afisa Habari wa Jeshi la Polisi Mkoa
wa Morogoro, Afande Suzy alisema wakiwa ofisini, walisikia harufu kali
hivyo kulazimika kufanya uchunguzi ndani na nje ya jengo hilo la polisi
lenye ghorofa moja ambapo chini zipo ofisi za Jeshi la Polisi Wilaya ya
Morogoro Mjini na juu za mkoa.
Wananchi wakiuopoa mwili wa Juma Mbega kutoka kwenye maji.
“Baada ya kuchunguza harufu hiyo, tulibaini uwepo wa maiti kwenye
kichaka kilichopo nje ya ofisi zetu ambapo mwili huo unaokadiriwa kuwepo
hapo kwa zaidi ya wiki moja ulikuwa umeharibika vibaya na kutoa harufu
kali,” alisema afisa huyo.
Kwa upande wake, Nuru Adam ambaye ni mjomba wa marehemu huyo,
akizungumza na gazeti hili eneo hilo la tukio alisema: “Huyu ni
mjomba’ngu, amezaliwa tumbo moja na mama yangu mzazi, Kilegu Hamis.
Simanzi baada ya kifo cha Mbega.
“Alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kuanguka hivyo huenda alikutwa na matatizo hayo akiwa eneo hili peke yake.”
Baada ya uchunguzi wa awali na ndugu wa marehemu kujulikana, maiti
ilichukuliwa na kupelekwa mochwari kuhifadhiwa huku taratibu za mazishi
kwa ndugu zikiendelea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment