Saturday, May 17, 2014
LOH!!! ONA JINSI WEMA NA AUNT EZEKIEL WALIVYOMFANYA JB......
IMEKULA kwake! Wauza nyago kwenye sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson wamemuingiza mkenge staa mwenzao, kaka mkubwa Jacob Steven ‘JB’ baada kukubali mwaliko kisha kumkatalia dakika za mwisho.
Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu.
Habari za ndani zilidadavua kwamba JB na wasanii hao walitakiwa kusafiri kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya kujifunza utamaduni wa huko ambapo walipelekwa na uongozi wa Ukumbi wa Princess Cassino uliopo Posta jijini Dar.
Katika hali ya kushangaza, uongozi huo ukiwa tayari umeshawakatia tiketi za daraja la kwanza (first class) zinazogharimu kama dola elfu moja (zaidi ya Sh. milioni 1.6) kila mmoja na baadhi ya wasanii kama Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ na Amri Athuman ‘Mzee Majuto’, Wema na Aunt Ezekiel walikataa siku moja kabla ya safari.
Diva kwenye tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel Grayson.
Chanzo chetu makini kilipenyeza habari kuwa, Wema na Aunt walichomoa safari hiyo baada ya kuhisi haikuwa na maslahi kwao na walivyopeleka maombi yao ya kimaslahi kwa JB, aliwaambia ni safari ya kujifurahisha na hakuna fedha yoyote watakayopata.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Aunt ambaye alikiri kuchomoa safari hiyo baada ya kushindwana kimaslahi.
“Unajua ile ni kwenda kutangaza biashara ya mtu kwa hiyo sisi tuliwatajia kiasi cha fedha ambacho tulikitaka kulipwa lakini tulishindwana ndiyo maana tukakataa kusafiri maana hatuwezi kufanya kitu ambacho hakina maslahi kwetu na kwenda kuwafaidisha wengine,” alifunguka Aunt.
Naye Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Nyerere’ aliilaani safari hiyo na kusema kwamba JB ni mnafiki kwani aliwachagua wasanii wachache kwa upendeleo ambao baadhi yao wamemwangusha kwa kutokwenda.
Jacob Steven "JB"
“Ukweli nimegundua JB ni mbinafsi, nilikuwa naambiwa lakini nikawa namtetea, sasa nimeamini kwamba hafai akirudi lazima nitamuita, nitazungumza naye kwa nini aliamua kufanya hivyo wakati kila kitu kinapotokea iwe safari au vitu vingine huwa sisi Bongo Movie Unity tunashirikishana lakini kwa hili ameona afanye mwenyewe,” alisema Steve Nyerere.
Labels:
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment