WASANII nyota wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na
Hisan Muya ‘Tino’ hivi karibuni walitiwa mbaroni katika mji wa Kilifi
ulio mbele ya Mombasa nchini Kenya baada ya kukutwa wakipiga picha za
filamu yao bila kuwa na kibali.
Msanii nyota wa filamu Bongo, Hisan Muya ‘Tino’.
Hata hivyo, waigizaji hao baadaye waliachiwa, ingawa hali ilikuwa
ngumu kidogo kwa Tino, ambaye polisi wa Kenya walidai hakuwa Mtanzania,
bali ni raia wa Somalia.
Dude alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema liliwatokea
kutokana na mazoea ya huku nyumbani ambako hufanya shughuli zao za
kupiga picha za filamu zao bila kuhitaji kibali.
Msanii nyota wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
“Yaani tumepata aibu ya mwaka, kwani tulienda kushuti bila kuomba kibali
kutokana na mazoea ya huku kwetu Bongo, tulipekuliwa sisi na gari letu,
baada ya hapo kibali kikaletwa nikaachiwa lakini Tino waliendelea
kumshikilia wakisema ni Msomali mpaka mkuu wa shirikisho la filamu
Mombasa alipokuja kuokoa jahazi, ukweli Kenya hakufai,”alisema Dude.
No comments:
Post a Comment