BAADA ya kuzagaa kwa taarifa mbalimbali kwamba
mwigizaji wa Bongo, Kajala Masanja anachepuka nje, ameibuka na kukanusha
madai hayo akisema hayana ukweli wowote.
Mwigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja
Mitandao mbalimbali ya kijamii imekuwa ikiposti taarifa mbalimbali
zinazomhusisha Kajala kutembea na wanaume tofauti kitu ambacho mwenyewe
amesema hakina ukweli na wanaosambaza uvumi huo, wakome.
Akizungumza na mwanahabari wetu Julai 3, mwaka huu alisema wanaoeneza
habari za yeye anachepuka wanamtafuta ubaya kwani hana mpango wowote wa
kuolewa wala kuishi na mwanaume kwa sasa.
“Waniache, mtu akisema nina mwanaume alishawahi kuniona? Sina mwanaume mwingine zaidi ya mume wangu,” alisema Kajala.
Kwenye mahojiano hayo, Kajala alisisitiza kuwa, haoni sababu ya yeye
kuchepuka wakati mumewe Faraja Augustino yupo hai na anaamini ipo siku
atatoka gerezani na ataendelea na maisha ya ndoa yake kama ilivyokuwa
zamani.
Kajala Masanja akiwa kwenye pozi
“Kiukweli sioni haja ya kuolewa na mwanaume mwingine tena wakati ni
wazi ipo siku mume wangu atakuwa huru, naomba ieleweke kwamba sina
mpango na mwanaume yeyote na sasa namgonjea atoke tuendelee na maisha
yetu,” alisema Kajala.
Mume wa Kajala, Faraja Agustino anatumikia kifungo cha miaka 7 baada
ya kushindwa kulipa faini ya shilingi milioni 200 kufuatia kesi ya
kutakatisha fedha iliyokuwa ikimkabili.
Kwenye kesi hiyo, Kajala
ambaye naye alihusishwa, alilipiwa faini ya shilingi milioni 13 na
mwigizaji Wema Sepetu, kifungo cha miaka mitano kikamuepuka.
No comments:
Post a Comment