Kijana alivyokuwa akipita barabarani bila woga.
Hapa yuko katikati ya barabara.
Akiendelea kuzunguka barabarani.
Hapa dereva alifanya juu-chini kumkwepa.
Ilikuwa ni hatari tupu kabla hajakamatwa na wenzake.
KIJANA mmoja aliyeonekana kuchanganyikiwa kutokana na kilichodaiwa ni
madawa ya kulevya, alionekana akitembea ovyo katikati ya barabara
maeneo ya Kamanyola, Sinza, jijini Dar es Salaam jana.
Kijana huyo alikuwa akikimbilia na kudandia magari yaliyokuwa
yanapita barabarani bila kuogopa chochote, jambo ambalo liliwachanganya
madereva.
Hata hivyo, vijana wenzake walioonekana kumfahamu walimkamata na kumpeleka kusikojulikana kwa ajili ya usalama wake.
No comments:
Post a Comment