Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Misri ,Cairo
kabla ya kufanyika kwa sherehe ya kumuapisha rasmi rais mpya wa taifa
hilo Abdel Fatah el Sisi.
Rais huyo mteule atakula kiapo chake cha kuchukua mamlaka katika mahakama kuu ya kikatiba mjini Cairo.Alishinda uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita kwa wingi wa kura ijapokuwa idadi ya waliojitokeza kushiriki katika shughuli hiyo ilikuwa chini ya asilimia 50.
Uchaguzi huo unajiri miezi michache tu baada ya kiongozi huyo kumpindua madarakani aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi.
Mkuu huyo wa jeshi wa zamani ameanzisha msako dhidi ya wanaompinga mbali na kukipiga marufuku chama cha Morsi cha Muslim Brotherhood.
No comments:
Post a Comment