BAADA
ya kudumu kwa zaidi ya miaka 10, imebainika kuwa ndoa ya mwanamuziki
mahiri wa muziki wa Injili Bongo, Flora na mumewe Emmanuel Mbasha ipo
chali kwa maana ya kuanguka huku ikidaiwa kuwa, kusimama imara tena
inawezekana lakini ni kazi kubwa.
Hilo limejitokeza wiki moja baada ya madai ya mwanaume huyo kudaiwa kumbaka shemeji yake na kesi ipo polisi.
Imeelezwa Flora na mumewe ambao walifunga ndoa Agosti 22, 2002
wamepita katika migogoro mizito lakini wawili hao walikuwa wakiyamaliza
kifamilia hadi kufikia hili la hivi karibuni ndilo lililoziba mataumaini
ya wawili hao kuishi kama mume na mke.
Chanzo kilicho karibu na wawili hao kimeeleza kuwa, mzizi wa wawili
hao kugombana ulichochewa na mwanamke mmoja (jina tunalo) ambaye alikuwa
akikinzana na ushauri wa Mbasha mara kwa mara.
“Kuna vitu Mbasha
alikuwa akimshauri huyo mama lakini walikuwa wakipishana Kiswahili na
hapo ndipo tatizo lilipokua hadi kufikia hatua ya kumwagana,” kilisema
chanzo.
Flora na mumewe Emmanuel Mbasha wakiwa kwenye pozi.
TUJIUNGE NA MBASHA
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Emmanuel alizungumza na mwandishi wetu
ambapo alikiri ndoa yake haina uhai tena na si rahisi kurejea katika
hali ya kawaida licha ya kudai kuwa bado anampenda mkewe.
“Tulikuwa tunagombana sana na Flora lakini tulikuwa tukipatana ila mama… (anamtaja jina) alichangia ugomvi,
Flora naye alikuwa na nyendo zake mbaya, kuna wakati alikuwa anatoka
kwenda gym (sehemu ya mazoezi) anachelewa kurudi ikafika wakati na nguvu
ya ndugu wa mke ikawa kubwa kiasi cha kunizidi mimi na hapo ndipo mambo
yalipofikia pabaya kabisa.”
FLORA ATIMKA NYUMBANI
Mbasha anaendelea: “Ugomvi
ulizidi, ilifika wakati tulipishana kiasi cha yeye kuondoka nyumbani na
kwenda kuishi katika nyumba ya wageni kwa miezi kadhaa wakati huo.
“Ndani ya ugomvi huo nilisikia mengi, baadhi ya watu wananiambia mke
wangu anaonekana na Prado na mwanaume mwingine mwenye pesa, iliniuma
sana ingawa sijawahi kumuona moja kwa moja,” alisema Emmanuel.
Kuhusu ugomvi huo, hivi karibuni Flora alikaririwa katika vyombo vya
habari akisema hana tatizo na mumewe na ameshasamehe na kusahau yote
yaliyopita hivyo ajitokeze tu ili akajibu mashitaka ya kudaiwa kubaka
binti wa miaka 17 yaliyofunguliwa.
“Mimi sina tatizo kabisa na mume wangu, nimeshasamehe yote
yaliyopita, kuhusu mashitaka ningeweza kuyafuta kama ningekuwa mimi
ndiye niliyemshitaki,” alisema Flora.
FLORA ADAIWA KUHAMIA KWA GWAJIMA
Wakati gazeti
hili likiendelea kusaka undani juu ya sakata hili, kuna chanzo kingine
kilipenyeza data kuwa baada ya ugomvi kuwa mzito, Flora alihamia kwa
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dar, Josephat Gwajima ambako
ndiko alikuwa akisali kila Jumapili.
“Kwani nyinyi Global hamna habari? Flora amehamia kwa Gwajima
Jumapili iliyopita, kwanza alihudhuria ibada jioni akaenda kuishi maana
Gwajima ni mchungaji wake kwa sasa,” kilisema chanzo.
GWAJIMA ACHOMOA
Ili kupata mizani ya madai hayo,
juzi Amani lilimpigia simu Mchungaji Gwajima na kumuuliza kama kweli
Flora amehamia kwake kufuatia ugomvi kati yake na mumewe ambapo alikataa
katakata.
“Flora hayupo hapa…mnataka niwaambiwe yuko hapa halafu
vyombo vya habari muanze kuandika vibaya? Hakuna kitu kama hicho,”
alisema Gwajima.
KWA NINI CHALI?
Ndoa kuwa chali ni ile ambayo
imeanguka lakini inaweza kusimama tena tofauti na ndoa kuvunjika. Global
iliwahi kuandika NDOA YA THEA CHALI baadaye ikasimama tena. Thea ni
msanii wa filamu alifunga ndoa na Michael Sangu ‘Mike’ ambaye pia ni
mwigizaji.
Flora na mumewe Emmanuel Mbasha wakilishana keki.
Wakati Emmanuel akizungumza na mwandishi wetu, alikiri kuwa Flora
ameshamgeuka na nguvu kubwa imemuingia ndani ya moyo wake hivyo kuna
ugumu sana wa kurudiana.
“Flora ambaye nilitegemea awe msaada katika hili lakini amefikia
steji ya kuacha kunisikiliza, anasema haniamini, kwamba ninaweza
kumfanyia lolote, sasa si bora kama anataka tuachane kwa heri kuliko
kuniundia zengwe ambalo linataka kunipeleka mimi jela?” alihoji Mbasha.
Kutokana na mvutano huo pamoja na kesi hiyo ya kudaiwa kubaka
inayomwandana Mbasha ni dhahiri kwamba kila mmoja hana imani na mwenzake
tena hivyo suala la wawili hao kuishi kama zamani linakuwa gumu kuliko
ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.
Emmanuel Mbasha alishitakiwa katika Kituo cha Polisi cha Tabata
Shule, Mei 30, mwaka huu kwa madai ya kumbaka shemejie.Uchunguzi juu ya
tukio hilo unaendelea hadi sasa shitaka ambalo mwenyewe amelikanusha.
No comments:
Post a Comment