Wednesday, June 11, 2014

MAJAMBAZI WALIOJIFANYA RAIA WEMA WAUA POLISI KIMANZI CHANA...... POLISI INAWASAKA WATUHUMIWA

Mwili wa askari polisi Joseph Ngonyani ukiwa katika hospitali ya wilaya ya Mkuranga.

Mnamo 11/06/14 majira ya 0100hrs
huko kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani,
watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia
wema waliingia kituo kidogo cha Polisi Kiman
nanzi Chana huku wakikimbia wakiwa na silaha
za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa
ni watu wanaohitaji msaada. Cha kushangaza
watu hao walimvamia askari mwenye silaha
ambaye amefahamika kwa jina la JOSEPH
NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga
na hatimaye kupora silaha SMG ikiwa na risasi
30. Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi
askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya
pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora
risasi za akiba 41 na kutoweka kusikojulikana.
Askari Ngonyani alifariki dunia alipokuwa
anapatiwa matibabu kwenye hospitali wilaya ya
Mkuranga. Askari mwingine aitwaye VENANCE
amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado
imo ndani, na kwenye paja la mguu wa kulia.
Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni
na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana
mateke na kujeruhiwa mbavuni. Kwa mujibu wa
mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo
aitwaye VERONICA MUSIME, anathibitisha
askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu
hapo Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa
Muhimbili kwa matibabu ya kina.

No comments:

Post a Comment