Gerald John Komba,jana aliamua kuvua gamba na kubwaga manyanga ya CCM na kujiunga na CHADEMA
Miezi kadhaa tangu mbunge wa Mbinga kwa tiketi ya CCM kapten John Komba
autangazie umma kwamba ataingia msituni kuanzisha vita iwapo mfumo wa
serikali 3 utapita,mtoto wake aitwaye Gerald John Komba,jana
aliamua kuvua gamba na kubwaga manyanga ya CCM na kujiunga na
CHADEMA,bwana Komba ambaye amehitimu shahada yake ya sheria chuo cha
SAUT mwaka jana alikuwa chuoni hapo kuchukua vyeti vyake vya elimu,ndipo
alipoamua kujiunga na CHADEMA tawi la SAUT,akizungumza na mwandishi wa
habari hii juu ya sababu zilizompelekea yeye kuamua kuachana na chama
cha babayake alisema
"Unajua ndugu yangu Kilunga,ukiwa chuo huwezi
ukayaona maisha halisi ya mtaani,mtaani ndo field kamili na ngumu,lakini
ukiwa chuo tena ukiwa mtoto wa kigogo huwezi ona umuhimu wa kuvisapoti
vyama vya upinzani,binafsi nimeenda nyumbani Mbinga na sehemu kadhaa za
nchi wananchi wanateseka sana,"alimaliza kuongea kijana huyo ambaye pia
anakipaji cha uimbaji kama babayake,alipoulizwa na mwandishi wa habari
hii kama anampango wa kwenda kumng'oa baba yake jimboni Mbinga kupitia
CDM alisema hilo lingewezekana akiwa CCM bt kwa CDM hafikirii kama hilo
linawezekana kwani CHADEMA hakuna sera za kurithishana majimbo ama
uongozi kama ilivyo kule CCM huku akitolea mfano wa majimbo ya Chalinze
na Kalenga,alipotakiwa azitolee ufafanuzi wa picha kadhaa zilizorushwa
mitandaoni zikimwonesha baba yake akiwa katika mikao tofauti ya
kimapenzi na binti mmoja alisema"japo katika siasa lolote linawezekana
bt kwa hili la picha nipo pamoja na mzee,picha zile hazina uhalisia bali
ni za kutengenezwa ili kumchafua mzee"
Haya yanatokea wakati ambao katibu wa itikadi na uenezi CCM Nape Moses Nnauye,akiutangazia
umma kwamba ameisambaratisha CDM chuoni SAUT kufuatia ziara yake
iliyofanyika siku 2 zilizopita na kufanikiwa kuwachukua wanachama wawili
waliokuwa tayari wamefukuzwa CDM SAUT kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo za
usaliti na kuhongwa pesa ili walivuruge tawi hilo la CHADEMA chuoni
hapo.
Picha chini aliyevaa shati la mistari ni Gerald Komba
alipokuwa akikabidhiwa kadi na katibu mwenezi wa tawi la SAUT ndugu
Jovinary Benson tawini hapo.
kweli hakuna mtu mwembembe,, hadi huyu jamaa kanenepa.. kweli ameanza kuwa mkubwa,, tangu enzi za mbezibeach high
ReplyDelete