Monday, June 2, 2014

CHRISS BROWN ATOKA JELA....

Mwanamuziki wa R&B wa nchini Marekani Chriss Brown

Mwimbaji nyota wa Marekani Chris Brown ameachiliwa kutoka gereza moja la Los Angeles.
Naibu Liwali wa LA, Tony Moore amesema mwimbaji huyo wa miondoko ya R&B ameachiliwa siku ya Jumatatu asubuhi.
Brown amekuwa gerezani tangu Machi 14, baada ya kuvunja sheria ya mahakama kuhusiana na kesi ya kumpiga mpenzi wake wa zamani, Rihanna mwaka 2009.

Chriss Brown akiwa na mpenzi wake, mwanamuziki Rihanna.

Kwa hisani ya Salim Kikeke

No comments:

Post a Comment