Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Asha (31) ambaye ni mke wa
mtu, amejikuta akiachika katika ndoa yake baada ya kudaiwa kumuunguza
midomo mwanaye, huko Yombo Buza, jijini Dar, Juni 24 mwaka huu.
Paulina, akiwa na majeraha ya moto midomoni.
Kwa mujibu wa majirani, mwanamke huyo alimchoma mtoto wake wa kumzaa,
Paulina, mwenye umri wa miaka mitano kwa kile alichodai kuwa tabia yake
ya kudokoadokoa fedha za mtaji wake wa biashara ya samaki.
Majirani hao walisema kuwa walimuona mama huyo akichochea moto wa
kuni katika jiko lililokuwa nje ya nyumba yake, kabla ya kuingia ndani
akiwa na fito moja inayowaka na muda mfupi baadaye wakasikia mtoto huyo
akilia kwa sauti iliyoonyesha kupata maumivu makali.
Kilio hicho kiliwashtua majirani hao ambao waliamua kuingia ndani ya
nyumba hiyo, lakini katika hali ya kushangaza, walimkuta mama huyo
ameshikilia kuni yenye moto huku mtoto huyo akiwa na majeraha ya
kuchomwa moto midomoni na mguuni.
Asha akijutia kitendo alichokifanya.
Baada ya kuona hivyo, walimshurutisha kuacha unyama huo na badala
yake ampeleke hospitali, lakini mama huyo alikataa katakata, akidai
hawezi kufanya hivyo hadi binti huyo mdogo atakapoacha tabia yake.
Kuona hivyo, majirani hao walitoa taarifa Kituo cha Polisi cha Buza
ambapo askari walifika eneo la tukio wakiongozana na mwanaharakati wa
haki za watoto kutoka taasisi binafsi ya Tuhimizane Children Academy,
Cleophas Simeone, ambao walimkamata na kumfikisha kituoni alikofunguliwa
jalada lenye namba CHA/RB/5521/2014, UKATILI DHIDI YA MTOTO.
Mwanaharakati huyo aliwasiliana kwa njia ya simu na baba mzazi wa
mtoto huyo aliyedai yupo nje ya Dar es Salaam kikazi ambapo baada ya
kusimuliwa kilichotokea, aliagiza mwanamke huyo kuondoka nyumbani kwake
muda huohuo na kumuomba Simeone aendelee kukaa na mwanaye ambaye
ameshaanza matibabu, hadi atakaporejea
No comments:
Post a Comment