Mabaki ya magari katika shambulio la Mpeketoni.
WATU watano wamepoteza maisha
baada ya shambulio lililotokea usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha
Pandanguo huko Witu wilayani Lamu nchini Kenya kilometa 30 kutoka
Mpeketoni yalipotokea mauaji ya watu zaidi ya 60 wiki iliyopita.
Polisi wamesema kuwa waliouawa ni kutoka jamii mbalimbali.
Mkuu wa
Polisi nchini Kenya, David Kimaiyo amesema kuwa washambuliaji walivamia
kijiji cha Pandanguo na kuua takribani watu watano.
"Bado tunawasaka waliohusika na shambulio hili, habari zaidi zitatolewa baadaye," alisema Kimaiyo.
No comments:
Post a Comment