WAKATI bado wananchi wakiwa wanajiuliza
kilichosababisha mama mkubwa wa mtoto Nasra Mvungi kumficha binti huyo
mwenye miaka minne ndani ya boksi, makubwa yameibuka kuhusu chanzo hasa
cha malezi hayo ya kudhalilisha.
Mtoto aliyedaiwa kuishi ndani
ya biksi kwa miaka mitatu akiwa na baba yake na kati ni Mama mkubwa wa
mtoto huyo Nasra Mvungi anayedaiwa kufanya kitendo hicho.
Mama mkubwa wa mtoto huyo Nasra Mvungi anayedaiwa kumficha mtoto huyo ndani ya boksi
Tukio hilo la aina yake lilitolea wiki iliyopita katika mtaa wa
Azimio, Kata ya Kiwanja cha Ndege mkoani hapa ambako wananchi walikwenda
hadi nyumbani kwa Mariam Said na mumewe Mtonga Omari na kuwafikisha
Kituo Kikuu cha Polisi Morogoro (Central Police) wakipinga mama huyo
kumtesa mtoto huyo anayedaiwa kuwa na ulemavu wa viungo.
Zoezi hilo lilifanyika Jumanne wiki hii, saa saba mchana ambapo
wananchi hao wakiongozwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo, Tatu
Mgagala walivamia nyumba hiyo na kumkuta mtoto huyo Nasra Rashid akiwa
stoo, ndani ya boksi huku mwili wake ukiwa na mabaka meusi, ikiashiria
kutoogeshwa kwa muda mrefu.
Nasra Mvungi akiwa chini ya ulinzi wa polisi
“lnauma sana, huyo mama na mumewe wanamtesa mtoto huyo kwa kumlaza
stoo kwenye boksi huku wakimlisha makombo, binafsi nilikuwa sifahamu
unyama huu, baadhi ya wananchi wangu wanaoishi jirani na familia hiyo
walikuja kwangu na kunieleza na mimi nikawataka twende wote
nikashuhudie,” alisema mwenyekiti huyo.
Walipomuuliza mwanamke huyo, alisema aliamua kumweka mtoto wa mdogo
wake stoo kutokana na baba mzazi kukataa kutoa fedha za matunzo, jambo
lililomkasirisha mume wake.
Baba mzazi wa mtoto huyo, Rashid Mvungi aliyejitambulisha kama Afisa
Ufundi ldara ya Elimu katika Halmashauri ya Mkoa wa Morogoro Vijijini
‘DED’ alikiri kumtambua Nasra na kutoa sababu za kushindwa kumlea ni
kuogopa familia yake kwani binti huyo yalikuwa ni matokeo ya mchepuko.
“Tulikubaliana na familia ya marehemu mzazi mwenzangu kuwa mama yake
mkubwa amtunze hadi atakapokuwa mkubwa, lakini nilikuwa sijui kama
anaishi katika mazingira kama haya,” alisema.
No comments:
Post a Comment