Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini katika moja ya kampeni zake za urais.
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameapishwa leo asubuhi jijini Pretoria kumalizia kipindi cha pili kama rais wa nchi hiyo yenye nguvu kiuchumi barani Afrika. Rais Zuma ameshinda uchaguzi uliomalizika hivi karibuni kwa ushindi mwembamba huku chama chake cha ANC kikikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwamo kushuka kwa uchumi wa nchi hiyo na ukosefu wa ajira kwa vijana.
Katika uchaguzi huo rais Zuma alijikuta akikabiliana na upinzani mkali kutoka kwa wanasiasa wa upinzani akiwemo mwanasiasa kijana Julius Malema aliyetimuliwa kutoka katika chama hicho na kuanzisha chama chake cha siasa kilichopata kuungwa mkono na vijana wengi pamoja na kuwa kichanga.
Baada ya kuapishwa rais Zuma anakabiliwa na changamoto kubwa ya kuimarisha uchumu wa taifa hilo tajiri.
No comments:
Post a Comment