Mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Francis.
Mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, amewasili Roma baada ya
kukamilisha ziara yake ya siku tatu Mashariki ya Kati ambapo alisema
kuwa tabia ya baadhi ya mapadri Wakatoliki waliokuwa wakiwanyanyasa
watoto wadogo kingono kanisani inaweza kulinganishwa tu na misa ya
Mashetani.
Baba Mtakatifu alifanya ziara ambayo ilihudhuriwa na maelfu ya watu
wa imani tofauti katika eneo hilo na wachambuzi wengi wamesema kuwa
imekuwa ya kufana.
Wengi wanasema kuwa Baba Mtakatifu kulinganisha vitendo vibaya vya
ngono walivyofanyiwa watoto na mapadri na misa ya mashetani ni lugha
nzito hasa ikitambuliwa kuwa tayari Papa Francis amewahi kuomba msamaha
kwa vitendo hivyo kote duniani.
Vitendo hivyo vimeharibia sifa Kanisa Katoliki kwa muda mrefu sasa.
Taarifa
kutoka makao makuu ya Papa yanasema kuwa kwa mara ya kwanza tangu yeye
achukue wadhifa wake anatarajiwa kukutana na wale walionyanyaswa na
mapadri kingono.
Wakatoliki wengi walikasirishwa na vitendo hivyo na
wamefurahi kuwa Papa anaweza kuomba msamaha na kisha akutane na
walioathirika na wengi wanasubiri kusikia atakachowambia atakapokutana
nao.
CHANZO BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment