Saturday, May 24, 2014

MWILI WA MAREHEMU AMINA NGALUMA WAWASILI DAR

Mwili  wa mwanamuziki Amina Ngaluma ukipokelewa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere ukitokea Thailand alipofia.

 Jeneza lenye mwili wa  Amina Ngaluma likiwekwa kwenye gari tayari kupelekwa kwa mumewe Kitunda.

 Mama mzazi wa Amina Ngaluma (kushoto) akilia kwa uchungu baada ya kuuona mwili wa mwanaye.

 Waombolezaji wakijadili jambo.

 Waombolezaji wakiwemo waandishi wa habari wakisubiri mwili wa marehemu Uwanja wa Ndege wa J ulius Nyerere Dar.

 Mume wa marehemu Amina, Rashid Sumuni ambaye pia ni mwanamuziki akiwa na huzuni uwanja wa ndege wakati anasubiri mwili wa mkewe.

 Mwanamuziki Mwijuma Muumini akihojiwa na mwanahabari kabla ya maiti haijafikishwa uwanja wa ndege Dar.

 Hatimaye mwili wa aliyekuwa mwanamuziki wa muziki wa dansi nchini Amina Ngaluma umewasili jana usiku jijini Da ukitokea nchini Thailand.
Mwili wa marehemu uliwasili kwa ndege ya  K.L.M  saa 4 kasoro robo  usiku wa jana, huku baadhi ya wadau wa muziki na wanandugu wakionesha kushangazwa na kitendo cha baadhi ya wanamuziki kutokufika katika kuupokea mwili wa Amina Ngaluma.
Kamera yetu ilishuhudia wasanii wachache waliowasili eneo la Uwanja wa Ndege akiwemo Mzee Cosmasi Chidumule na Mwijuma Muumini ambaye alitoka Kahama kwa ajili ya kuudhuria mazishi ya mwanamuziki huyo anayetarajiwa kuzikwa leo mchana.

No comments:

Post a Comment