Maskini! Wakati tasnia ya filamu Bongo ikiwa katika majonzi ya
kuondokewa na ‘dairekta’ na mwigizaji mkubwa, Adam Phillip Kuambiana
(38), pigo lingine limetokea kwa wasanii hao kwa kuondokewa na kichwa
kingine, Sheila Haule ‘Recho’ (26). Recho alikutwa na umauti Mei 26,
mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar alipokuwa amelazwa
baada ya kujifungua kwa oparesheni Mei 25, mwaka huu kwenye Hospitali
ya Lugalo, Dar.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo marehemu Rachel Haule ‘Recho’ enzi za uhai wake.
KUJIFUNGUA
Kwa mujibu wa chanzo makini
kilichokuwepo kwenye Hospitali ya Lugalo, Recho alikuwa akisumbuliwa na
tatizo la presha ya kupanda, kisukari na kifafa cha mimba.
Chanzo hicho kilieleza kuwa, kwa zaidi ya saa 23 tangu afikishwe
hospitalini hapo, Recho aliteseka kwani madaktari walikuwa wakihangaika
kuishusha presha ili kuweza kunusuru uhai wake hivyo staa huyo
alipigania uhai wake kwa masikitiko makubwa.
“Tulipomfikisha alifanyiwa vipimo, ikagundulika ana tatizo la presha
na kisukari na hata alipojifungua alipata kifafa cha mimba ndipo hali
ilipozidi kuwa mbaya,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya
jina.
UTABIRI WA KUAMBIANA
Chanzo hicho kilizidi
kueleza kuwa, pamoja na jitihada za madaktari kuhakikisha wanaokoa
maisha ya mwigizaji huyo na mwanaye, walifanikiwa kumfanyia oparesheni,
mtoto wa kiume akatoka salama lakini muda mchache baadaye alifariki
dunia huku Recho akiwa katika hali mbaya.
Kwenye gazeti la Amani lililopita toleo namba 814 la Mei 22, mwaka
huu, kulikuwa na habari iliyomhusu Recho juu ya marehemu Kuambiana
aliyemtabiria kuwa atajifungua mtoto wa kiume iliyokuwa na kichwa cha
habari kilichosomeka: “Kuambiana alimtabiria mtoto Recho”.
Recho Haule akiwa kwenye pozi.
Katika habari hiyo, Recho alieleza namna alivyokutana na Kuambiana na
kumtabiria kuwa atajifungua mtoto wa kikume, kweli ikatimia kwani
alijifungua mtoto huyo lakini bahati mbaya alifariki dunia hivyo kuacha
huzuni kubwa.
Utabiri huo ulipotimia Jumapili iliyopita, uliibua simanzi nzito kwa
baadhi ya wasanii hasa baada ya mtoto kufariki dunia huku wengi wao
wakikumbuka utabiri alioutoa Kuambiana.
KUHAMISHIWA MUHIMBILI
Baada ya madaktari wa
Lugalo kuona tatizo linazidi, Jumatatu iliyopita walilazimika kumhamisha
Recho katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alilazwa katika
chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
“Ilibidi apewe ‘transfer’ ya kwenda Muhimbili kwani hali yake haikuwa
nzuri hasa baada ya kujifungua na kupata kifafa cha mimba, akalazwa
ICU,” kilisema chanzo hicho.
MADAKTARI WAMFICHA MCHUMBA’KE
Taarifa kutoka
Muhimbili zilidai kwamba baada ya kuona umati wa wasanii wa Bongo Movies
usiku hospitalini hapo, madaktari walilazimika kumficha mchumba wake,
George Saguda pamoja na wasanii wengine kwani walitambua pigo
walilolipata hivi karibuni kwa kuondokewa na mwigizaji Kuambiana.
“Waliona watawaongezea majonzi kwa kuwapa taarifa za msiba hivyo
wakalazimika kuwaficha hadi Jumanne asubuhi ndipo wakatoa taarifa za
kifo,” alisema nesi mmoja wa Muhimbili bila kutaja jina.
ODAMA ABAKI NA SIRI NZITO
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Recho na shosti yake kipenzi, Jennifer Kyaka ‘Odama’ wawili hao walikuwa watu wa karibu mno.
Ilielezwa kwamba Recho na Odama walikuwa wakishirikiana kwa kila jambo hivyo atakuwa amebaki na siri nzito Recho.
“Marehemu amemuachia siri nzito sana Odama, walikuwa wakishirikiana
katika kila kitu na kutunziana siri nyingi nje ya kazi ya sanaa,”
kilisema chanzo hicho.
Recho alilelewa na bibi yake baada ya kufiwa na wazazi wake wote
hivyo mipango ya kumsafirisha marehemu iliendelea kufanyika juzi Jumanne
ambapo wasanii walitarajia kuchangisha shilingi milioni kumi
kufanikisha shughuli ya kuaga, majeneza (mama na mtoto) na kusafarisha
msiba kwenda nyumbani kwao Songea, leo Alhamisi.
Mpaka Recho anapatwa na umauti, alikuwa akijulikana zaidi kwa jina la
Rachel Haule lakini kwa mujibu wa mama yake mdogo ambaye jina
halikupatikana, marehemu alibatizwa kwa jina la Sheila Haule.
Recho aliyezaliwa 1988, aliingia kwenye fani ya uigizaji mwaka 2009.
Baadhi ya filamu alizocheza ni pamoja na Loreen, Unpredictable, Danger
Zone, Men’s Day Out, Vanessa (yak wake mwenyewe na nyingine. Fuata
makala ukurasa wa 9. Sisi wote tu mavumbi, mavumbini tutarejea. Mungu
ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
No comments:
Post a Comment