Friday, May 23, 2014

IRENE UWOYA AFUNIKA UTURUKI..... YASEMEKANA NI MMOJA WA WASANII WAKALI WA KIKE AFRIKA...

                  Mkali wa Bongo Movie, Irene Uwoya.

Msanii wa filamu Tanzania, Irene Uwoya amefunika katika ziara yao inayoendelea nchini Uturuki. Katika ziara hiyo ambayo imedhaminiwa na Princess casino ya Dar Es Salaam Uwoya ameongozana na baadhi ya wasanii wengine wa filamu akiwemo Vincent Kigosi "Ray", Amri Athumani "King Majuto" na Jacob Steven "JB" ambaye amerejea hivi karibuni kuwahi mazishi ya muigizaji mwenzao Adam Kuambiana.

Baadhi ya wasanii na watayarishaji wa filamu nchini humo wamemwagia sifa Irene Uwoya hasa kwa kazi nzuri aliyoifanya katika filamu ya "Off Side" akishirikaina na baadhi ya wasanii marufu nchini akiwemo marehemu Steven Kanumba. Mmmoja wa watayarishaji wa filamu alisema kwamba iwapo filamu hiyo ingekuwa bado haijatoka basi wangeweza kuifanyia marekebisho kidogo na kuiingiza katika soko na kimataifa na ingeweza kuingiza mabilioni ya pesa.

Irene Uwoya katika moja ya Scene za movie ya Off Side akiwa na marehemu Steven Kanumba.

Hapa ni Irene Uwoya akiwa na nguli wa Bongo Movie, JB katika moja ya scene za filamu ya Off Side.

No comments:

Post a Comment