Hadi gazeti hili linaondoka kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira
Maria Mama wa Mkombozi, Sinza jijini Dar juzi saa 10:00 jioni, ndoa ya
Mbunge Vicky Kamata iliyokuwa ifungwe hapo iliyeyuka.
Vicky Kamata akiwa na Charles walipokuwa matembezini nchini China.
Vicky Kamata ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya UVCCM,
Mkoa wa Geita alikuwa afunge ndoa na mwanaume aliyejulikana kwa jina la
Charles wa jijini Dar.
KATEKISTA AZUNGUMZA NA IJUMAA WIKIENDA
Baada ya
kuona muda unakwenda bila kuwepo kwa dalili za wahusika kufika kufunga
ndoa hiyo ambayo harusi yake ilidaiwa ingetumia shilingi milioni 96,
wanahabari wetu walimtafuta Baba Paroko, Cuthbert Maganga ili kumsikia
anasema nini kuhusu hilo.
Hata hivyo, mtu aliyedai ni katekista wa kanisa hilo alisema paroko alikwenda hija, Buguruni, Dar.
Kuhusu ndoa ya Vicky Kamata, katekista huyo alidai Jumapili ya Mei 18,
2014 ndani ya ibada za kanisa hilo ilitangazwa hadharani ‘laivu’ kwamba
haitafungwa.
Vicky Kamata akiwa amelazwa baada ya kuugua ghafla katika Hospitali ya Tabata General jijini Dar.
SABABU ZA KANISA
Habari za ndani zilidai kuwa kanisa lilibaini upungufu mkubwa kwa bibi harusi na kumwambia ndoa haitakuwepo.
Upungufu huo ni pamoja na Vicky Kamata kushindwa kuwasilisha cheti
chake cha ubatizo, pia hakuwahi kupata kipaimara. Ilidaiwa kuwa vitu
hivyo kwa uchache wake ni kikwazo kikubwa kwa mtu kufikia daraja la
Sakramenti ya Ndoa.
SABABU ZA NDANI
Ukiachana na sababu hizo za
kanisa, Ijumaa Wikienda lilichimbua na kubaini sababu kuu 3 ambazo
zilikuwa kisiki cha kufungwa kwa ndoa hiyo.
Vicky na Charles wakila bata.
SABABU YA KWANZA
Kwa mujibu wa chanzo, mwanaume
aliyetaka kufunga ndoa na Vicky ana ndoa nyingine ya kanisa na imejaliwa
kupata watoto kadhaa hivyo isingekuwa rahisi kufungwa kwa ndoa nyingine
kwa mujibu wa maandiko ya Biblia. Mume mmoja mke mmoja mpaka kifo
kiwatenganishe.
MKE ATINGA BUNGENI
Chanzo kilizidi kudai kuwa
wiki iliyopita, mwanamke huyo ambaye jina halikupatikana, alitinga
bungeni na kuonana na Spika wa Bunge, Anne Makinda ambapo
alijitambulisha ndiye mke wa Charles anayetaka kufunga ndoa na Vicky
Kamata.
“Mke wa bwana harusi alikuja Dodoma juzi, akasaidiwa kuonana na spika na mbunge mmoja (jina tunalo).
“Alimwambia spika yeye ndiye mke wa ndoa wa Charles, ila walitengana.
Lakini alisema pamoja na kutengana huko, ndoa ya Kikristo haifungwi
mara mbili labda mmoja afe. Kwa hiyo mumewe hawezi kufunga ndoa na
Vicky,” kilisema chanzo.
SABABU YA PILI
Sababu ya pili ilielezwa kuwa,
Vicky asingeweza kufunga ndoa hiyo kwani mwanaume huyo alishatoa mahari
kwa msichana mmoja (jina tunalo) wa jijini Dar na ukweni anajulikana.
“Alishatoa mahari kwa msichana mwingine mbali na Vicky, ukweni anajulikana.
Vicky Kamata akiwa katika pozi na mwanaume aliyepanga kuoana naye anayejulikana kwa jina la Charles wa jijini Dar.
“Sasa ilipotoka ile picha yake kwa mara ya kwanza kwenye Gezeti la
Ijumaa (Mei 16, 2014) yenye kichwa cha habari ndoa ya Vicky itatumia
shilingi milioni 96 ikawa kasheshe kwa yule msichana na ukweni, ndiyo
jamaa akaamua kutangaza kubatilisha ndoa na Vicky,” kilisema chanzo.
SABABU YA TATU
Sababu ya tatu ilitajwa ni
kitendo cha kuumwa. Wikiendi iliyopita, Vicky aliugua ghafla na kulazwa
katika Hospitali ya Tabata General jijini Dar kwa hiyo isingekuwa rahisi
ndoa kufungwa Jumamosi kutokana na hali yake kuwa mbaya.
WAANDISHI WATINGA HISPITALI
Ijumaa iliyopita,
waandishi wetu walitinga kwenye hospitali hiyo na kukutana na daktari
mmoja ambaye alikiri Vicky kulazwa hapo lakini alikataa waandishi
wasimuone kwa sababu hayuko katika hali nzuri kiafya. “Ni kweli Vicky
kalazwa hapa lakini hamuwezi kumwona, hayuko katika hali nzuri,
anahitaji kupumzika jamani, please,” alisema daktari huyo.
HATIHATI ILISHAKUWEPO
Katika Gazeti la Uwazi la
Mei 20, 2014 ukurasa wa mbele kulikuwa na habari ndogo yenye kichwa
kisemacho; NDOA YA MIL. 96 YA VICKY KAMATA HATIHATI KUFUNGWA.
Katika habari hiyo ilielezwa kuwa ndoa hiyo isingefungwa kutokana na kuibuka kwa mizengwe kibao.
Habari za ndani zilisema mizengwe hiyo iliibuka katika hatua za mwisho
na kusababisha mwanaume kuamua kubatilisha ndoa hiyo ambayo ilikuwa
ifungwe Mei 24, mwaka huu jijini Dar.
KIONGOZI MKUBWA SERIKALINI
Ilidaiwa kuwa baada
ya kuibuka kwa zengwe na mume kutangaza ndoa basi, Vicky aliumia na
kuzifikisha habari hizo kwa Spika Makinda ambapo naye alizifikisha kwa
kiongozi mmoja mkubwa serikalini, hasa bungeni.
Kiongozi huyo alichukua jukumu la kumvutia waya bwana harusi na
kumsihi kutochukua mawazo hayo na ikibidi ndoa ifungwe lakini mwanaume
huyo alikataa katakata akisema mambo hayo ni ya kifamilia zaidi kwa hiyo
yaachwe kwenye familia.
MAMA SITTA ASIKITIKA
Habari zinazidi kusema kuwa
kati ya watu ambao wamehuzunishwa na kutofungwa kwa ndoa hiyo ni Mbunge
wa Viti Maalum (CCM), mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta ambaye
aliposikia kuyeyuka kwa ndoa hiyo alisikitika si kwa sababu alikuwa
kwenye vikao vya harusi, bali pia aliuona wakati mgumu atakaoupata Mhe.
Vicky.
WABUNGE WAULIZIA MICHANGO YAO
Pamoja na yote
yaliyojitokeza, habari zinadai kwamba baadhi ya wabunge waliochanga pesa
ili kufanikisha harusi hiyo tangu juzi wameanza kuulizia michango yao
wataipataje kwa vile harusi basi tena!
“Huku Dom (Dodoma) hakukaliki bwana. Baadhi ya wabunge wameanza
kuulizia michango yao, wanasema kama harusi haipo basi na chao
wakipate,” alisema mbunge mmoja akiomba kuhifadhiwa jina.
WABUNGE WATAJWA KUINJINIA
Mbunge huyo alikwenda
mbali zaidi kwa kusema kuwa kuna wabunge wametajwa ‘kuinjia’ zengwe la
kutokufungwa kwa ndoa hiyo kwa sababu wanazozijua wao ambazo Ijumaa
Wikienda haikupewa lakini inaendelea kuzichimba.
VICKY KAMATA
Vicky alipotafuwa kwa njia ya simu Jumamosi iliyopita ili azungumze lolote kuhusu kuyeyuka kwa ndoa yake hakupatikana hewani.
No comments:
Post a Comment