Adam Phillip Kuambiana enzi za uhai wake akiwa amevaa shati alilonaswa nalo
AMA kweli duniani kuna sarakasi! Takribani siku kumi tangu alipofariki
dunia aliyekuwa ‘kichwa’ kwenye filamu za Kibongo, Adam Phillip
Kuambiana (38), mrembo aliyejitambulisha kwa jina Mary Njombe amenaswa
na nguo za staa huyo wakati mali za marehemu hazijagawanywa.
Mary Njombe aliyenaswa akiwa amevaa nguo za marehemu Adam Phillip Kuambiana.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu makini, Mary ambaye ni mkazi wa Magomeni
Hospitali, Dar amekuwa akipigilia pamba za marehemu hasa baada ya jamaa
huyo kutangulia mbele ya haki.
“Jamani njooni huku Magomeni
Hospitali hapa mtaa wa pili kuna mwanamke anatinga nguo za marehemu
Kuambiana,” kilisema chanzo chetu.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu walifanya msako eneo hilo hadi wakamnasa Mary.
Katika mahojiano na gazeti hili, Mary alisema kuwa alikuwa mchumba wa
Kuambiana na alichobahatika kubaki nacho ni nguo ambazo alimpatia mara
ya mwisho amfulie (zinaonekana pichani).
Mary alisema kuwa yeye na Kuambiana walifahamiana tangu mwaka 2006 ambapo alikuwa akimbembeleza kuwa naye.
“Mwaka 2008 ndiyo tulianza rasmi uhusiano kwani mimi nilikuwa sina
mwanaume na yeye hakuwa na mtu hivyo tulikubaliana na alikuwa
akijulikana nyumbani kwetu,” alifunguka Mary.
Mwanadada huyo alisema kuwa yeye na Kuambiana walikuwa wakikutana
kwenye Hoteli ya Grand iliyopo Magomeni, Dar na mara nyingi alikuwa
akimpikia chakula na kumpelekea ‘lokesheni’.
“Nimeumia sana na
sijielewi, Kuambiana ameniachia donda kubwa, nakumbuka neno la mwisho
aliniambia nimpende sana kwani ipo siku nitamkubuka,” alisema Mary huku
akiangua kilio.
Adam Phillip Kuambiana enzi za uhai wake akiwa amevaa shati alilonaswa nalo mrembo.
Alipoulizwa kama kweli nguo hizo ni za marehemu Kuambiana, alizama ndani
akatoka akiwa amevaa pensi na shati la ‘drafti’ alilokuwa anapendelea
kulivaa staa huyo ambalo ni maarufu sana.
Kuambiana alifariki dunia
usiku wa kuamkia Mei 17, mwaka huu baada ya kuanguka chooni kutokana na
kusumbuliwa vidinda vya tumbo.
No comments:
Post a Comment