MWIGIZAJI na Muongozaji filamu maarufu Bongo, Adam Kuambiana amefariki dunia wakati akipelekwa hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam kwa matibabu alfajiri ya kuamkia leo. Marehemu alianguka chooni akiwa location katika hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remy, Dar. Kabla ya mauti kumfika, Adam alikuwa akilalamika kuwa anasumbuliwa na tumbo. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!
Adam Kuambiana akiwa na Irene Uwoya
Marehemu Adam Kuambiana akiwa na waigizaji wenzake wa Bongo Movie
Fake Pastors ni moja kati ya filamu za kwanza kabisa kumpa umaarufu marehemu Kuambiana.
Tasnia ya Filamu na Taifa kwa ujumla tutakukumbuka daima Adam Kuambiana.
No comments:
Post a Comment