Tuesday, May 13, 2014

BOKO HARAM WATOA VIDEO YA WASICHANA WALIOWATEKA... INGIA HAPA UITAZAME LIVE BILA CHENGA.....

Hawa ndiyo wasichana waliotekwa na magaidi wa Boko Haram wa Nigeria

Masaa machache yaliyopita kiongozi wa kundi hatari la magaidi la Boko Haram, Abubakar Shekau ametoa video inayowaonesha wasichana wa chibok waliotekwa na kushikiliwa na kundi hilo wiki chache zilizopita katika eneo la Borno kaskazini magharibi mwa Nigeria. Abubar Shekau ametoa video hiyo na kuitaka serikali ya Nigeria kuwaachia baadhi ya wanamgambo wa kundi hilo wanaoshikiliwa kuachiwa ili nao waweze kuwaachia wasichana hao.




Pia Shekau ameongeza kuwa wasichana wote wamebadilishwa dini na kuwa waislamu na hawataachiwa huru mpaka wanamgambo wote wa Boko Haram watakapoachiliwa na serikali ya Nigeria.

Wasichana wawili kati ya kundi hilo la wasichana waliokuwa wamevalia hijabu walisema kwamba mwanzoni walikuwa wakristo lakini sasa wamebadilishwa dini na kuwa waislamu.

No comments:

Post a Comment